Fun-Lugha

Your ever reliable language services provider in Tanzania

LESSON #35: Hadithi, Hadithi…#1 (Kiama cha Mkopaji)

Hadithi, hadithi” is the phrase most Swahili story tellers use when they start telling a story (‘hadithi’ just means story) & that’s why I named this segment just that.

Kiama Cha Mkopaji

Hapo zamani za kale palikuwa na mzee mmoja aitwae Kanyawi ambaye alihamia kijiji cha Ntenga kutoka Usambaani.Mzee huyu alikuwa anapenda sana kunywa pombe na hata alipomaliza fedha zake zote aliamua kuweka rehani chochote alichonacho. Hakika mzee huyu alikuwa kero sana kwa familia yake kwani kila aliyekopwa alifika nyumbani kwake na kudai deni lao. Kutokana na heshima waliyokuwa nayo watoto wake na mke wake; walilazimika kulipa madeni mara kwa mara. Ilifikia wakati ambapo mke na watoto wote ilibidi kubuni miradi mbalimbali ili waweze kulipa madeni na kusomeshana. Mtoto mkubwa aliyeitwa Mwasu alibuni mradi wa kufuga nyuki na hivyo kuchonga mizinga ya nyuki mizuri sana pale kijijini.
Siku moja kama ilivyokuwa kawaida ya Mzee Kanyawi; alikopa tena pombe ya dengelua yenye thamani ya shilingi elfu tatu. Baada ya kudaiwa alimuambia aliyemkopesha kuwa afike nyumbani kwake kesho yake ili ampe fedha zake. Keshoye yule aliyemkopesha alimpigia mzee Kanyawi simu kuwa yupo njiani kwenda kuchukua fedha zake.
Mzee kanyawi kusikia hivyo aliangalia juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yake na kuona mzinga mpya wa nyuki ambao bado haujaingliwa na nyuki na kumwambia mke wake kuwa kuna watu wanakuja kumuua na hivyo ataingia ndani ya ule mzinga na afungiwe mle ili wale wanaomdai wasimuone. Kutokana na upendo mkubwa kwa mumewe alikubali ombi lile na kumfungia mumewe ndani ya mzinga wa nyuki. Punde si punde yule mzee Mwasu alifika na kuulizia alipokuwa mzee Kanyawi. Mke wake alimtetea na kusema kasafiri ghafla hadi wiki ijayo. Mzee Mwasu alisononeka sana na kuamua kuchukua ule mzinga uliokuwa juu bila kujua kuwa yule mzee alikuwa ndani yake na kuondoka nao hadi nyumbani kwake. Alipofika kwake Mzee Mwasu aliulizwa na mkewe iwapo alifanikiwa kupata fedha zile na kumwambia kuwa hakumkuta lakini aliamua kuchukua mzinga wake mpya ili waupasue na kupata kuni za kupikia kwani yule mzee sio mlipaji. Mzee Mwasu alimtaka kijana wake wa kazi achukue shoka na kupasua ule mzinga ili wapate kuni za kupikia chakula. Hadi hapo yule mzee Kanyawi alikuwa kimya ndani ya mzinga akisubiri jioni ili atoke na kurudi kwake.
Kijana yule wa “miraba minne” alichuka shoka na kulishushia kwenye mzinga ule na “ghafla” damu zilitapakaa kila mahali. Walipoangalia vizuri waliona kuwa ni yule mzee Kanyawi kapasuliwa kichwa. AMA KWELI KIAMA CHA MKOPAJI KILIMTOA ROHO BILA KUOMBA MAJI.

                                                    XXXXXXX MWISHO XXXXXX

(Hadithi hii imetungwa na Sekiete Mtana. Darasa la sita Shule ya Msingi Ushindi- This story has been written by Sekiete Mtana of Ushindi Primary School (Std. 6))

Words and phrases:

Kiama cha mkopaji- the final judgement/the end of the (frequent) borrower
Hapo zamani za kale- once upon a time
Mzee (wazee)– an old man (although most older men say from about 45 years old are usually referred to as ‘mzee’ as well, as a form of respect)
Kijiji (vijiji)- village
Pombe- alcohol
Fedha- money
Kuweka rehani- to pawn
Kero- bother
Deni (madeni)- debt
Kubuni- to come up with, to create, to invent…
Kufuga nyuki- bee keeping
Mizinga ya nyuki (mzinga wa nyuki)- beehives
Siku moja– one day
Thamani- value
Upendo- love
Punde si punde- soon
Ghafla- suddenly
Alisononeka- he was saddened
Kuni- firewood
Kijana (wake) wa kazi- (his) house help
Shoka (mashoka)- axe
Kijana yule wa ‘miraba minne’- that well built young man (‘miraba minne’ literally means 4 squares…mmmhhh???…chin scratch…)
Damu zilitapakaa- blood spread/splattered
Mwisho- the end

Click the link below to listen to the story being read and pick up on pronunciation of the various words…

EPISODE 31: Hadithi, Hadithi…#1.

Advertisements

Single Post Navigation

Your Thoughts...

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: