Fun-Lugha

Your ever reliable language services provider in Tanzania

Translation Challenge #6… (swa-eng)

Nina furaha sana kusherehekea mwaka mmoja tangu tovuti hii kuanzishwa. Kusema ukweli sikuanza na matarajio makubwa, nilitaka tu kuwaonyesha wanafunzi wangu sampuli za mbinu ninazotumia kufundisha na pia kuwapa watu wasiojua Kiswahili ladha kidogo tu ya lugha hii, yani tunaita kionjo. Mwanzoni watu walikuwa wanakuja tu wanachungulia wanaondoka, bila hata kuniachia mawazo yao. Ila sasanafurahi sana ninapoona watu wanaambiana juu ya tovuti hii, wanawasiliana nami kupitia mitandao ya jamii na wengine hata kuniweka kwenye orodha ya vifaa vya kujifunza Kiswahili (http://www.fb10.uni-bremen.de/khwagner/swahili/links/gesamt.aspx, http://kamusi.org/content/swahili-learning-resources)……sielewi Kijerumani ila natumaini wameandika mambo mazuri tu!

Asanteni sana kina Boga, Joyce Keeley, Madebe na wengine wote wanaozidi kutembelea na kurusha maswali, “komenti” nk. zinazonisaidia kuboresha ninachokiandika hapa. Inshallah tutasherehekea hata miaka kumi na zaidi ila kwa sasa ntashukuru tu tukifikisha mwaka wa pili.

Mungu ibariki Fun-Lugha!

Advertisements

Single Post Navigation

Your Thoughts...

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: